Alhamisi , 21st Sep , 2023

Mwili wa msanii kutoka Nigeria "Mohbad" umefukuliwa huku raia wa nchi hiyo wakitaka uchunguzi wa mwili wake ufanyike kutokana na chanzo cha kifo chake ikidaiwa ameshambuliwa na kuwekea sumu kabla ya umauti kumfika. 

Picha ya Mohbad na kufukuliwa kwa mwili wake

Mwili huo umefukuliwa baada ya suala hili kuzidi kuwa kubwa na kuibua maandamo maeneo mbalimbali Nigeria ya kudai haki juu ya kifo cha Mohbad na watu hawakupendezwa na kitendo cha kuzikwa mapema kabla ya uchunguzi. 

Mohbad alifariki Sept 12 kwa sababu inayotajwa kuwa ni msongo wa mawazo na infection. Alizikwa siku iliyofuata, Septemba 13.