
Korea Kaskazini ina nia ya kushirikiana na Urusi katika maeneo ya usafiri wa anga
Baada ya chakula cha jioni katika mkutano huo, kiongozi huyo wa Urusi aligonga glasi ya mvinyo na Kim kuashiria urafiki wa nchi hizo mbili. Kim alisema "tutaendelea kuunga mkono maamuzi ya Rais Putin na ... tutakuwa pamoja katika vita dhidi ya ubeberu"
Putin amesema Urusi itaisaidia Korea Kaskazini kutengeneza setilaiti baada ya Korea Kaskazini kushindwa mara mbili mwaka huu kuzirusha.
Viongozi hao hawakuzungumzia hatari ya vita vya nyuklia, msemaji wa Kremlin anaongeza.
kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi Interfax, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema,
Mazungumzo ya Rais Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yalikuwa "muhimu na yenye maana",
Akizungumza baada ya viongozi hao wawili kufanya mazungumzo katika eneo la Mashariki ya Mbali la Urusi, Peskov aliongeza kuwa Korea Kaskazini ina nia ya kushirikiana na Urusi katika maeneo ya usafiri wa anga