Jumanne , 12th Sep , 2023

Bondia Mtanzania Hassani Mwakinyo Leo jumanne ya Septemba 12,2023 amepimwa afya kuelekea katika pambano la Kimataifa la mkanda wa ubingwa wa IBA dhidi ya Mkenya Rayton Okwiri Litakalokuwa raundi 10 ambalo linatarajiwa kufanyika Septemba 29,2023 mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kupimwa Afya yake ,Bondia Mwakinyo amesema kuwa amejiandaa vyema hakika itakuwa ni sikukuu ya Taifa hivyo mashabiki wake wajitokeze kwa wingi.

“Nilikaa nje kwa muda mrefu hivyo wapenzi wa ngumi watarajie kuona burudani ya aina yake kutok kwangu nimejiandaa kushinda “amesema Mwakinyo.

Kwa upande mwingine Bondia Mwakinyo ametoa Pongeza kwa Rais wa serikali ya Mapinduzji  ya Zanzibar  Dokta Hussein Mwinyi  kwa kurudisha mchezo wa ngumi Visiwani Zanzibar.