
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Pia amemuagiza Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Tandahimba Deogratius Mbowe amuhoji Afisa Kilimo wa Kata ya Kitama, Sharaf Manjavila kwa tuhuma za kuchukua pembejeo za wakulima.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Agosti 13, 2023, wakati akiongea na wananchi baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Kitama wilayani Tandahimba mkoani Mtwara.
Awali, baadhi ya wananchi walimuomba Waziri Mkuu aondoke na Afisa Kilimo huyo kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake ikiwemo kumtuhumu kuiba pembejeo za wakulima wa korosho.
Wakulima hao walidai kuwa walifanyiwa uhakiki na kupewa namba ila wanapokwenda kuchukua pembejeo wanaambiwa hawajasajiliwa na majina yao hayajarudi, hivyo hawapewi dawa.