Ijumaa , 2nd Jan , 2015

Chama cha Mpira wa Magongo Mkoa wa Dar es salaam DRHA kimesema kinatarajia kuongeza shule ambazo watakuwa wanatoa mafunzo kwa vijanja ili kuweza kukuza mchezo huo kwa vijana.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa DRHA, Mnonda Magani amesema wameshapeleka barua katika shule zaidi ya saba katika wilaya ya Ilala ambapo wanatarajia kuongeza katika shule za wilaya ya Temeke na Kinondoni ili kuweza kupata vijana wengi zaidi watakaoweza kupata mafunzo ya mchezo huo.

Magani amesema, Progamu hiyo wanatarajia kuisambaza mpaka katika mikoa mbalimbali nchini lakini kwa sasa wameanza na Dar es salaam kutokana na wingi wa shule zilizopo.

Magani amesema, kila mchezo unaendana na miundombinu yake, hivyo bado wanaendelea kufuatilia suala la viwanja ili kuweza kupata shule nyingi zaidi zitakazoweza kushiriki.