Wakulima wadogo na wafugaji kutoka mikoa yote nchini wanakutana mkoani Morogoro kujadili Katiba iliyopendekezwa, iwapo imezingatia maslahi ya wazalishaji wadogo.
Mkurugenzi wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania, MVIWATA Stephen Ruvuga , akizungumza mjini Morogoro, amesema pamoja na Katiba hiyo iliyopendekezwa kuangalia suala la haki za ardhi kwa wakulima bado wanaona haki zilizopo hazitoshelezi.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Deus Kibamba, akiwaasa wananchi kuepuka maneno ya kuonesha kuiomba serikali kufanya jambo kupitia katiba, hali inayoweza kuzua mtafaruku kama uliotaka kujitokeza bungeni pale kamati ya bunge ilipozozana na serikali ikitaka baadhi ya mikataba.
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Eliya Ntandu amewaasa wakulima na wafugaji kuwa na ushirikiano usio wa kisiasa ili kuweza kusaidiana sambamba na makundi hayo kuwa na umoja wenye nguvu ili kuongeza uzalishaji na kuboresha soko la ndani, huku wakulima na wafugaji wakilalamikia mifugo kufa nyakati za kiangazi kwa kukosa mvua kutokana na uharibifu wa mazingira hususani ukataji wa miti ovyo.