Ijumaa , 28th Mei , 2021

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa vyuo vya ufundi nchini kutumia fursa ya maonesho ya ufundi kujitathimini kazi wanaoifanya kama imefikia kiwango cha kuweza kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya mtungi wa kuzima moto kutoka Mkuu wa Chuo cha Zimamoto kilichopo Ilala Dar es salaam, Kenedy Komba katika Maoneosho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Akizungumza wakati akifungua maonesho ya ya pili ya elimu ya mafunzo ya ufundi yalifonyaki jijini Dodoma leo Mei 28, 2021, Mhe. Majaliwa amesema bado serikali inahitaji mfumo rasmi wa kuandaa vijana katika viwango vya juu vya mahalifa na stadi za kutenda.

“Nitoe wito kwa vyuo vyetu vya ufundi kutumia fursa hii vizuri katika kuona kazi wanazozifanya na mafanikio wanayoyapata katika kazi hiyo nakufanya tathimni ili kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuajiri wenzao,“ amesema Mhe. Majaliwa.

“Elimu ya ufundi ni mkakati mzuri utakaosaidia kubadili fikra na mitazamo ya raia wetu ili waweza kuelimika na kuwa mahiri katika stadi za maarifa kusaidia kukabiliana na changamoto za maendeleo ya nchi yetu,” aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa

Aidha, Mhe. Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ili kukuza ujuzi kwa watu wote huku akisema serikali ipo wazi kuwasikiliza.

Waziri Mkuu Majaliwa amefungua rasmi maonyesho ya pili ya elimu ya  mafunzo ya ufundi, ambayo yatafanyika kwa siku saba Jijini Dodoma huku akitoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.