Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.
Jengo hilo linalo tazamana na Bustani ya Forodhani ni jengo kubwa na refu zaidi katika eneo la Stone Town na ni miongoni mwa majengo ya zamani yaliyo jengwa mwaka 1883 na baadaye kufanyiwa ukarabati miaka ya karibuni.
Akizungumza leo Disemba 28, 2020 alipokutana na wadau kutoka Mji Mkongwe Rais Mwinyi amesema kuwa, tume atakayoiteua kufanya uchunguzi huo haitakuwa na lengo la kuonea watu ila itasaidia kuupata ukweli wa chanzo.
“Tusubiri ripoti itatupa picha kamili ya kilichosababisha madhara yale, tuiache tume ya uchunguzi ifanye kazi yake, tume nitakayoteua kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha jengo hilo kuporomoka, ilete ripoti ya kweli itakayotusaidia na itasaidia kutoleta madhara tena”, amesema Dkt. Mwinyi.
Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa, “Inatakiwa wataalam watuelekeze mara moja kuwa ni majengo yapi yafungwe mara moja kabla hayajaleta maafa, ili tufahamu ni majengo gani yatafaa kwaajili ya Mji Mkongwe, tume ile haitakuwa na lengo la kumtuhumu mtu yeyote, nia yetu ni kujenga sio kubomoa ila tutakapogundua uzembe hatutosita kuchukua hatua”.
Jengo la ghorofa maarufu Bait al-Ajaaib kabla ya kuporomoka
House of Wonders lilikuwa miongoni mwa majengo sita ya Ikulu na makazi ya zamani ya Sultan wa pili wa Zanzibar, Barghash bin Said, enzi za ukoloni na biashara, katika karne ya 17.
House of Wonders kwa sasa lilikuwa limefungwa kutumika kutokana na sehemu kubwa ya jengo hilo kupasuka na kuharibika na kuanguka roshani yake mwaka 2012 kisha kuanguka paa la jengo hilo mwaka 2015. Jengo la ghorofa maarufu Bait al-Ajaaib baada ya kuanguka.