Baada ya kucheza na kinara wa Kundi Al Hilal mwenye alama 10, Yanga watarejea Nyumbani kucheza dhidi ya MC Alger mwenye alama 5 Januari 18/2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kuelekea mchezo wa tarehe 12 Yanga itawakosa Maxi Nzengeli, Yao Kouassi pamoja na Aziz Andambwile ambao ni majeruhi.
Kikosi cha Yanga SC kinatarajia kushuka dimbani Januari 12/2025 kucheza mchezo wa Kundi A Ligi ya mabingwa barani Afrika katika Uwanja wa Stade Cheikha Ould Boidiya, Nouakchott nchini Mauritania dhidi ya Al Hilal Omdurman. Yanga inahitaji kushinda michezo yote miwili iliyosalia ili kufikisha alama 10 katika kundi A na kujihakikishia kufuzu hatua ya robo fainali ambapo mpaka sasa imekusanya alama 4 katika michezo 3.
Baada ya kucheza na kinara wa Kundi Al Hilal mwenye alama 10, Yanga watarejea Nyumbani kucheza dhidi ya MC Alger mwenye alama 5 Januari 18/2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kuelekea mchezo wa tarehe 12 Yanga itawakosa Maxi Nzengeli, Yao Kouassi pamoja na Aziz Andambwile ambao ni majeruhi.
Kikosi cha Wanachi kimeondoka Alfajiri ya leo kikiwa kwenye hali nzuri na ari kubwa ya kupambana ili kujihakikishia kusalia kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu huu.Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania bara sambamba na kombe la CRDB Conferation imeondoka ikiwa na imani kubwa ya kushinda mchezo wake wa siku ya Jumapili ili kujihakikishia kufuzu kucheza robo fainali ya michuani hiyo.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani haina matokeo mazuri inapocheza ugenini dhidi ya Wababe hao wa Sudan.Lakini Yanga SC imefanya vizuri msimu wa 2022-2023 iliocheza fainali ya kombe la shirikisho ilishinda michezo yake ya ugenini ikiwemo iliyokutana na timu kutoka ukanda wa Afrika ya Kaskazini.
Yanga SC haijapoteza mchezo katika mashindano yote tangu ipoteze michezo mitatu mfululizo ya ligi kuu Tanzania bara na klabu bingwa Afrika dhidi ya Al-Hilal Club (Omdurman) ya nchini Sudani mchezo uliochezwa dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.Safu ya ushambuliaji wa vijana wa Jangwani imerejesha makali yake hivyo kuufanya mchezo wake dhidi ya Al Hilal uwe wa kuvutia kuutazama.