Job Ndugai, Spika wa Bunge la 12.
Katika uchaguzi uliofanyika hii leo Novemba 10, 2020, Bungeni Dodoma, Ndugai amepigiwa kura na wabunge wateule 344 kati ya wabunge 345 na kura ya hapana ilikuwa ni moja.
Awali akiomba kura kwa wabunge hao, Ndugai amesema kuwa Bunge la 12 litakuwa ni Bunge bora na lenye mfano wa kuigwa kuliko mabunge yoyote yale na kwamba katika Bunge hilo hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni kwa kuwa hawajatimiza asilimia 12.5, kwa mujibu wa kanuni za Bunge.