Jumatano , 29th Oct , 2014

Hatimaye Rapa Chid Benz leo amefanikiwa kupata dhamana na kutolewa rumande na kurejea uraiani.

Chidi Benz akiwa chini ya ulinzi

Hii ni baada ya staa huyu kutimiza masharti aliyowekewa kwa dhamana hiyo, ambayo ni wadhamini wawili wa kuaminika na shilingi milioni 1.

Msanii huyu anatakiwa kufika mahakamani tena tarehe 11 mwezi Novemba ambapo kesi yake itatajwa tena.

Tags: