Thomas Ulimwengu akiwa na TP Mazembe
Ulimwengu amerejea Mazembe ambako aliondoka mwaka 2016 kwenda kutafuta mafanikio mengine ya soka barani Ulaya, ambapo alijiunga na klabu ya FC Athletic Eskilstuna kisha FK Sloboda Tuzla kati ya mwaka 2017-18.
Mwaka 2018 alirejea barani Afrika ambapo alijiunga na klabu ya Al Hilal of Omdurman na baadaye mwaka 2019 alijiunga na klabu ya JS Saoura ya Algeria ambapo alicheza katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na kikosi hicho.
Ulimwengu anarejea kuimarisha safu ya ushambuliaji ya TP Mazembe, ambapo anatarajia kutua mjini Lubumbashi Jumatano, Januari 28 kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.