Jumamosi , 28th Dec , 2019

Watu watatu wamefariki Dunia katika matukio matatu tofauti yaliyotokea wakati wa Sikukuu ya Krismasi katika Wilaya za Muleba, Bukoba na Ngara mkoani Kagera, akiwemo mtoto Everine Method mwenye umri wa miaka 13, mwanafunzi wa Shule ya msingi Kagoma, ambaye mwili wake ulikutwa kichakani.

Maharage

Akizungumzia matukio yaliyotokea wakati wa Sikukuu ya Krismasi, Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa tukio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Kagoma wilayani Muleba.

Kamanda Malimi amesema kuwa mtoto huyo ametumwa na shangazi yake aliyekuwa akiishi naye, kwenda kuvuna Maharage kwa ajili ya mboga, lakini hakurejea hadi maiti yake ilipokutwa katika kichaka na Mzee Tryphone Katabaro aliyekuwa akichunga mbuzi.

Kuhusu tukio la pili Kamanda Malimi amesema kuwa Johan Japhet mwenye umri wa miaka 38, mwili wake uligundulika kandokando mwa njia katika Kijiji cha Nakatunga wilayani Ngara, na kuwa tukio la tatu ni la mtembea kwa mguu Pauline Karugira mkazi wa Mtaa Bugombe, katika Mansipaa ya Bukoba, aliyepoteza maisha baada ya kugongwa na chombo cha moto ambacho hakijafahamika kama ni pikipiki