Chid Benz ameiambia EATV & EA Radio Digital,kuwa hakuna kitu kikubwa anachoweza kukizungumzia zaidi tu ya kuwa Shetta ni mdogo wake.
"Ni mdogo wangu wa Ilala amezaliwa namuona nyumbani kwao, kama walivyokuwa wadogo zangu wengine na wengine hakuna kitu maalumu kuhusu Shetta, kitu maalumu ni amezaliwa kutoka Ilala mtaani anakua akiwa Shule namuona" ameeleza Chid Benz.
"Mimi ni kaka yake huwezi kusema akina Shetta wanakupa support gani, wale tupo tu tunaishi maisha kama maisha ya kifamilia, tunaweza tukabadilisha mada tafadhali " ameongeza.
Chid Benz amekuwa akihusishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya, ambayo yamemfanya kupoteza afya yake pamoja na kushindwa kurudi katika hali yake ya zamani.