Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt Shukuru Kawambwa
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph kilichoko jijini Arusha wamegoma kuingia madarasani kwa madai kwamba mitaala wanayotumia sio ya fani ya ualimu wanayosomea bali ni ya masomo ya uhandisi
EATV imefika katika chuo hicho na kuzungumza na wanafunzi hao ambao wanasema baada ya kuwauliza walimu wao juu ya tatizo hilo waliwajibu kuwa wawaulize watendaji wa shule kwani wao hawajasomea ualimu bali wamesomea uhandisi.
Pia wanafunzi hao wamesema wamekuwa wakipewa mafunzo kwa vitendo yasiyo na hadhi ya vyuo vikuu na pia baadhi ya mambo ya msingi yanayohusiana na fani yao hawajayasoma na mengine hayapo kabisa jambo wanaloliona kuwa kama litaendelea watamaliza muda wao bila kupata elimu waliyoitarajia.
Mwakilishi wa viongozi wa shule hiyo ambaye ni mhadhiri msaidizi Bw, Josephate itambu amekiri kupokea malalamiko ya wanafunzi hao na kwamba wameyafikisha panapo husika kwani wao ni watendaji na hawawezi kuzungumzia masuala ya utawala
Jitihada za kuwatafuta viongozi na chuo hicho chenye wanafunzi zaidi ya 700 na watendaji wa wenye dhamana ya elimu ili wazungumzie suala hilo zinaendelea.