Jumanne , 25th Dec , 2018

Baadhi ya wananchi Mkoani Geita wamesherehekea siku ya sikukuu ya kuzaliwa Yesu Kristu (Krismasi), kuelekea mwaka mpya huku wakiwa na furaha kubwa ya kuona Tanzania inaingia kukuza uchumi Barani Afrika kwa kufufua Shirika la Ndege ATCL ambalo wanaamini litaingizia nchi mapato makubwa.

Ndege ya Tanzania A220-300

Kauli hiyo ya wakazi wa Geita imekuja siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza mamia ya watamzania kupokea ndege ya Tanzania aina ya aina A220-300 ambapo viongozi mbali wa kitaifa walishiriki zoezi hilo.

Akizungumza mkoani Geita na www.eatv.tv, Richard Nzagamba mmoja wa wakazi wa Geita amesema mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na hatua ya serikali ya awamu tano kuamua kujitegemea kiuchumi bila ya kutegemea misaada ya mataifa mengine, huku wakikumbana na vikwazo na masharti magumu ya kimkataba.

Kwa upande wake Nzagamba na Methew Daniel wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kumtaka kuzidi kutekeleza ahadi zake alizozitoa mwaka 2015.