Jumatatu , 14th Jul , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Malfred Alfred ameweza kukonga nyoyo za mashabiki katika tamasha kubwa la muziki liliobatizwa jina Jugend-festival Iller-tissen 2014 lililofanyika hivi karibuni nchini Ujerumani.

Msanii wa bongo Malfred Alfred

Malfred ameiambia eNewz kuwa hii imekuwa ni nafasi kubwa kwake kwa kupata mwaliko huo akiwa kama mgeni kutoka barani Afrika ambapo ameweza kupaform jukwaa moja na bendi maarufu za nchini humo zikiwemo 'like the Killerpilze' na 'Qunstwerk!!

Aidha Malfred ameelezea kuwa hivi sasa anaendelea kuutangaza muziki wake nchini Ujerumani huku akiwa amefanya kolabo mpya na msanii Kala Jeremiah katika wimbo wao mpya uliobatizwa jina 'Usipoteze Time.