Alhamisi , 9th Jan , 2025

Tanzania inashika nafasi ya tatu katika nchi zinazofanya vizuri kwenye ubora wa ngumi za kulipwa barani Afrika kwa mujibu wa taarifa ya viwango vilivyotolewa January 2025 na  shirikisho la mkanda wa ABU.

Mchezo wa ndondi unakua kwa haraka nchini Tanzania pamoja na kuongeza Mashabiki wapya kutokana na nguvu kubwa inayotumika kuutangaza mchezo huo.Mafaniko ya Bondia Hassan Mwakinyo yamewafanya Vijana wengi kuuona mchezo wa ndoni kama sehemu ya kuweza kubadili maisha yao na ya Familia zao.

ABU chini ya mwenyekiti  Houcine Houichi imeitaja Afrika kusini namba moja baada ya   kuingiza mabondia wengi kwenye vipengele mbalimbali vya orodha hiyo pia imeingiza idadi kubwa ya mabondia kuliko Nigeria na Tanzania ambazo zimepisha kidogo.

Taifa hilo limeingiza mabondia 36 kwenye jumla vipengele 16 kati ya vipengele 18 ,Nigeria mabondia 18 kwenye vingele  13  huku Tanzania imekua ya tatu baada ya kuingiza mabondia 18 kwenye vipengele 11 kati ya vipengele vyote 18 vya madaraja tofauti ya kila uzito.

Mchezo wa ndondi unakua kwa haraka nchini Tanzania pamoja na kuongeza Mashabiki wapya kutokana na nguvu kubwa inayotumika kuutangaza mchezo huo.Mafaniko ya Bondia Hassan Mwakinyo yamewafanya Vijana wengi kuuona mchezo wa ndoni kama sehemu ya kuweza kubadili maisha yao na ya Familia zao.

Majina mengi makubwa yamewahi kusikika nchini Tanzania kwenye tathinia ya ngumi lakini hawakuwa na mafanikio makubwa kimaisha kama Wapiganaji wa sasa.Mabondia kama Maneno Osward Mtambo wa Gongo, Rashidi Matumla Snake Boy na Francis Cheka yalikuwa ni majina makubwa Tanzania kwenye ngumi lakini hawakupata mafaniko makubwa ya Kifedha.

Uwekezaji unaendelea kufanyika kwenye masumbwi nchini unazidi kuvutia Vijana wengi kuupenda nchezo huo na Wazazi kuona kuna haja ya kuruhusu Watoto wao kucheza mchezo huo kutokana na fedha zinazomiminika kwa Mabondia kwasasa.