Pichani ni Rais wa 47 wa taifa la Marekani Bw. Donald Trump ambaye anatarajiwa kukabidhiwa rasmi kofia hiyo mapema jumatatu 20 January 2025
Mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya ByteDance, unashambuliwa na mamlaka za juu ikiwemo mahakama, kwa kile wanachodai kuwa usalama wa taarifa za watumiaji wa mtandao huo kutokea nchini Marekani kuwa mdogo.
Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao ''X'' wa mtengeneza maudhui maarufu mtandaoni Mr Beast ameweka wazi nia yake ya kutamani kununua mtandao huo ili usifungiwe kwa nchini Marekani.
Mtandao wa TikTok kwa sasa una zaidi ya watumiaji milioni 170 nchini Marekani, na ifikapo tarehe 19 mtumiaji wa TikTok kutokea nchini humo itamlazimu kutumia huduma ya VPN ili kuficha utambulisho wake ndipo aweze kutumia mtandao huo.