Picha yamfanya Nisha kutaka kuolewa na Ommy Dimpoz

Jumatatu , 10th Mei , 2021

Unaambia picha ya Ommy Dimpoz imemfanya msanii wa filamu Nisha Bebe kutamani kuolewa na msanii huyo wa muziki wa BongoFleva ambaye kwa sasa yupo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kuhiji.

Msanii Ommy Dimpoz kulia, kushoto ni Nisha Bebe

Nisha Bebe amesema Ommy Dimpoz amefanya kitu kikubwa sana na amemshawishi na yeye kwenda kufanya tukio hilo la kuhiji Mjini Mecca, Saudi Arabia kama alivyokuwa anafanya marehemu Mzee Majuto.

"Yaani sijawahi kuona picha ya mtu nikatamani kuolewa naye, mara baada tu ya kuiona hii picha nimetamani kuolewa na Ommy Dimpoz na ni kitu ambacho hata akilini mwangu hakikuwepo,umefanya kitu kikubwa sana"

"Serious wa kwanza kunishawishi kutamani kuhiji ni marehemu baba yangu Mzee Majuto, Ommy leo umenikumbusha vitu vingi sana, kiukweli nimejiskia raha kutoka moyoni kwa hiki ulichofanya" ameongeza

Pia amemtaka Ommy Dimpoz asirudie makosa aliyowahi kuyafanya na aendelee kuishi kwenye mstari ulionyooka mpaka mwisho wa maisha yake.