Jumamosi , 19th Mei , 2018

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu Simba SC wameshindwa kufurukuta mbele ya Kagera Sugar ambao wamevunja rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuwafunga mabingwa hao msimu huu.

Kagera Sugar ambayo imepachika goli dakika ya 86 ya mchezo katika lango la Simba ambalo limeipa pointi tatu na kuwa na jumla ya Pointi 34.

Awali kabla ya mchezo kuanza Nyota wa Kagera Sugar walisema kuwa licha ya kwamba wapinzani wao wameshatwaa Ubingwa, lakini watahakikisha wanashinda mchezo huo ili kuwatibulia sherehe yao jambo ambalo wamefanikiwa kulitimiza

Timu ya Simba imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kuwa na alama 68 kwenye mechi 29 ambazo haziwezi kufikiwa na Azam FC yenye alama 52 kwenye mechi 28 wala Yanga yenye alama 48 kwenye mechi 26.