Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda.
Mhe. Makinda amesema hayo wakati akizindua kitengo maalumu cha kuchuja na kusafisha damu nchini kwa wagonjwa wa figo, katika Hospitali ya Hubert Kairuki iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo kitengo ambacho kina mashine pekee ya kufanya shughuli hiyo kwa haraka na usalama kwa mgonjwa mwenye uhitaji na kuokoa maisha yake.
"Wanasiasa na viongozi muache tabia ya kuwavunja moyo wa kufanya kazi wataalamu maana wana uwezo mkubwa kama madaktari bingwa wa magonjwa wanaofanya kazi zao nje ya nchi hivyo ni vyema kuwatia moyo wa kufanya kazi ili kuingia kwenye ushindani wa kutibu magonjwa sugu duniani", amesema Mama Makinda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Hubert Kairuki, Dkt. Asser Mchomvu amesema mbali na teknolojia hiyo bado wanakumbana na changamoto za wataalamu bingwa wa magonjwa kama ya figo na kuchuja damu.