Jumamosi , 5th Apr , 2025

Klabu ya Simba imethibitisha kumualika Mtume Boniface Mwamposa (Buldoza) kama moja ya wageni wake siku ya Jumatano katika mchezo wa awamu ya pili ya robo fainali ya Kombe la shirikisho Barani Afrika, mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa.

Mtume Boniface Mwamposa (Buldoza)

Simba inatafuta nafasi ya kufuzu hatua ya Nusu fainali baada ya kupoteza kwa magoli mawili kwa sifuri nchini Misri katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa hatua ya robo fainali. Kupitia mitandao yao ya kijamii Simba wameandika ujumbe unaosema;

"Safari hii tumedhamiria Ubaya Ubwela na tunamualika kila mtu mwenye mchango mkubwa kwenye jamii hii, wacahwi wengi ndugu zangu, kuna watu wamekunja nafsi kwelikweli”

“Kwa mantiki hiyo namtangaza mgeni mwingine maalumu Mtume Boniface Mwamposa (Buldoza). Tunafanya mazungumzo naye pia ikiwezekana kesho tukawauzie waumini wake tiketi."- Semaji Ahmed Ally akiongea na Wanasimba wa Ukonga Mazizini.