
Bukayo Saka
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alifanyiwa upasuaji wa tatizo la misuli ya paja alilolipata katika mchezo wa Ligi dhidi ya Crystal Palace Desemba 21.
Saka, ambaye amefunga mabao tisa na kutoa asisti 10 katika mechi 24 katika michuano yote msimu huu akiwa na Arsenal, anaweza kushiriki katika mechi ya Jumanne dhidi ya Fulham kwenye Uwanja wa Emirates.
“Bukayo Saka yuko tayari kucheza, ni wakati sahihi kumtumia, Bukayo ni silaha kubwa ambayo tunayo. Tunajua athari aliyonayo katika timu, mchango wake ni muhimu kwa mafanikio yetu."-Kocha Mikel Arteta
Arsenal wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, wakiwa na tofauti ya alama 12 dhidi ya vinara Liverpool huku wakiwa wamesalia na mechi tisa kutamatika kwa msimu wa 2024/25.