Jumanne , 1st Apr , 2025

Jeshi la China linasema limeanza mazoezi ya pamoja ya vikosi vyake vya ardhini, wanamaji, na maroketi kuzunguka kisiwa cha Taiwan.

Beijing imesema mazoezi hayo ni onyo la wazi dhidi ya harakati za Taiwan kujitangazia uhuru, ikimuita Rais La Ching wa kisiwa hicho kuwa ni kupe.

Jeshi hilo limesema kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa WeChat, kwamba mazoezi hayo yanalenga kuonesha utayari wa vikosi vyake hivyo kufanya doria ya baharini na angani, kutwaa udhibiti kamili na kuweka vizuizi kwenye maeneo muhimu.

China, ambayo kamwe haijaondowa uwezekano wa kutumia nguvu kuitwaa Taiwan, imekuwa ikiongeza shinikizo lake la kijeshi na kisiasa dhidi ya kisiwa hicho katika miaka ya hivi karibuni.