Alhamisi , 3rd Apr , 2025

FIFA imetoa orodha ya viwango vya Dunia kwa timu za taifa upande wa Wanaume hii leo Alhamisi, Aprili 3, ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 106 viwango vilivyopita mpaka nafasi ya 107 viwango vya sasa.

FIFA imetoa orodha ya viwango vya Dunia kwa timu za taifa upande wa Wanaume hii leo Alhamisi, Aprili 3, ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 106 viwango vilivyopita mpaka nafasi ya 107 viwango vya sasa. Majirani zetu Uganda wameshika nafasi ya 89 huku Kenya wameshika nafasi ya 111 kidunia.

Morocco imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya 14 hadi ya 12 huku kwa Afrika wakishika nafasi ya kwanza. Senegal nafasi ya 19, Misiri nafasi ya 32, Algeria 36 katika viwango vya dunia kwa sasa.

Ureno ya Cristiano Ronaldo imeshuka hadi nafasi ya saba huku Uholanzi ikichukua nafasi ya bingwa huyo wa Euro 2016 katika nafasi ya sita. Kwa upande mwingine, bingwa mtetezi wa Uropa Uhispania amechukua nafasi ya mshindi wa zamani wa Kombe la Dunia Ufaransa nafasi ya 2 kidunia.

Mataifa mengine katika 10 Bora kwa viwango vya sasa namba moja ni Argetina, nafasi ya pili ni Uhispania, nafasi ya 3 imekamatwa na Ufaransa, huku namba 4 England, namba 5 Brazil, nafasi ya 6 Uholanzi, namba 7 Ureno, namba 8 ni Ubeligiji, nafasi ya 9 ni Italy huku nafasi 10 imefungwa na Ujerumani.