moja kati ya mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara
Bodi ya ligi kuu Tanzania TPLB imetoa ushauri kwa wachezaji na vilabu katika kuelekea mchakato wa zoezi la usajili ambalo linataratarajia kuanza june 15 mwaka huu
Mtendaji mkuu wa bodi hiyo Silas Mwakibingwa amesema katika maswala ya usajili hasa wachezaji wanatakiwa kuwa makini hasa linapofika suala la kuingia mikataba na klabu inayomuhitaji mchezaji.
Mwakibinga amesema mikataba katika soka la kisasa ni masuala ya kisheria na hivyo amewataka wachezaji kuwatumia wanasheria ili wapate ushauri wa kisheria badala ya kuangalia gharama kwani kutofanya hivyo watakuwa wakikosa haki zao kutokana na wao kutojua sheria