Ben Sanane - Kada wa CHADEMA anayedaiwa kutoweka
Akiongea na vyombo mbalimbali vya habari hii leo Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu amesema, Msaidizi huyo Bwana Ben Sanane hajaonekana kwa muda sasa hivyo kuiomba serikali kupitia Jeshi la Polisi Tanzania kuwapa taarifa kwani tayari wamekwisha toa taarifa ya kupotea kwa jeshi hilo.
Mhe. Lissu amesema wanaingiwa na hofu kuhusiana na tukio la kupotea kwa kada wao huyo hivyo ushirikiano wa kutosha na jeshi la polisi unahitajika katika kuwasaidia kupata jibu ni wapi alipo kada huyo na kuweza kutambua kama bado yupo hai.
Tundu Lissu - Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA