Miongoni mwa watakaokabidhi tuzo kesho ni Tbway 360 kutoka 5Selekt ya EATV akiwa nyota wa Bongo Movie, Lulu
Tunaweza kusema kuwa kila kitu kiko 'mguu sawa' maana kila idara imejipanga kuanzia wasanii watakaoperfom, wasanii wanaowania tuzo, waratibu wa shughuli nzima, na wote watakaohusika kubwa ikiwa ni waandaaji wa ukumbi utakaotumiwa siku ya kesho.
Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha maandalizi ya ukumbi kwa siku ya leo ambao timu nzima ya wahusika ilikuwepo kufanya mazoezi (reheasal)
Stage katika hatua za mwisho za maandalizi
Host wa tukio hilo, Salama J, naye akiwa 'mguu sawa' kuandika historia
dancers katika maandalizi
Joachim Mabula - moja kati ya mashabiki wa EATv waliojipatia zawadi ya tiketi kuandika historia
Viti viko tayari kukaliwa, pia kuandika historia
Maeneo maalum ya kulia bata ndani ya ukumbi wa Mlimani City (juu na kulia) , kushoto ni maandalizi ya dancers
Baadhi ya wasanii wanaowania tuzo wakiwa ndani ya ukumbi
Wasanii wanaowania tuzo wakiitest stage
Kabla ya kuingia ndani, hili ni eneo maalum kwa ajili ya kujiselfisha na mastaa
Bei ya tiketi ni Shilingi 20,000 kwa 50,000 endapo utanunua katika vituo vya mauzo lakini endapo utanunua kwa njia ya M Pesa, tiketi zinakuwa ni shilingi 18,000 na shilingi 45,000/-