Bi. Helen Siria - Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka Barclays
Akizungumza na EATV Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka Barclays Bi. Helen Siria, amesema wanaishukuru EATV kwa kuwapa fursa hiyo ya kukutana na vijana hivyo baada ya kumaliza mafunzo ambayo wameyaandaa kwa vijana watatoa tiketi 20, ili waweze kuhudhuria usiku wa #EATVAwards.
Hivi sasa benki ya Barclays wanaendesha kampeni yao ya #ReadyToWork ambayo inawalenga wanafunzi na kutoa mafunzo ya kuweza kujiajiri, inayoendeshwa Afrika nzima.
Mtazame hapa akielezea kampeni hiyo kwa undani na jinsi ya kushiriki https://youtu.be/MgSK5Y8SBMc