Jumatatu , 28th Nov , 2016

Ongezeko kubwa la idadi ya watu kila mwaka nchini Tanzania imeipa hofu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini katika kushugulikia changamoto za afya zinazoikabili sekta hiyo

Dkt. Hamis Kigwangalla

Sababu ya hofu hiyo ni kuwa ongezeko hilo linahitaji maboresho makubwa ili kufanikiwa kuwahudumia wananchi kikamilifu kulingana na mahitaji na idadi yao.

Akiongea na East Afrika Radio mara baada ya kumalizika kwa mjadala ulioandaliwa na ubalozi wa Uswizi ili kuihoji serikali juu ya namna ambavyo inajidhatiti kuboresha upatikanaji endelevu wa huduma bora za afya nchini Naibu Waziri Wa Afya Mhe. Hamis Kigwangala amekiri kuwa idadi kubwa ya ongezeko la watu linahatarisha upatikanaji wa huduma za afya hivyo inawapasa kutenga fedha nyingi zaidi

Mhe, Kigwangala amesema, ni lazima serikali ijiandae kwa upande wa lazingira ya namna itakavyo wapatia huduma mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula, ajira na huduma bora za afya kwani ongezeko hilo nikubwa zaidi endapo watanzania watakuwa zaidi ya millioni 100 miaka ijayo.

"Tuko mbioni kuunda sheria ambayo itawezesha wananchi wote kuwa na bima ya afya ili kuwezesha idadi kubwa ya watu walioko kwenye makundi maalum ya kupewa msamaha wa matibabu kama vile wagonjwa wa saratani, watoto wadogo, kina mama wajawazito na wazee waweze kumudu kuhudumiwa na serikali" amesema.

Sikiliza hapa