Joh Makini (Kushoto) na Sam Misago
Ngoma hiyo imemuigiza Joh katika tuzo hizo kupitia vipenge viwili ambavyo ni Wimbo Bora wa Mwaka na Video Bora ya Mwaka.
Katika katika kipindi cha FNL cha EATV, Mwamba wa Kaskazini amesema amejisikia furaha na faraja kwa kiasi kikubwa kuona kazi yake inathaminiwa na kuingizwa katika tuzo hizo kubwa za muziki na filamu Afrika Mashariki, huku akiimwagia sifa EATV kwa kuthamini muziki wa Tanzania na kuanzisha tuzo hizo.
Pia, Joh a.k.a Mwamba wa Kaskazini hakusita kuufagilia muziki wa hip hop nchini Tanzania kwa kusema kuwa muziki huo ndiyo wenye nguvu zaidi kwa kuwa wasanii wake wengi ni wabunifu
"Muziki wa hip hop kuingia kwenye category za tuzo hizi ni sawa na kuipa hip hop heshima, tena ilitakiwa nyimbo za hiphop ziwe kwenye kila category" amesema Joh.
Akizungumzia mabadiliko ya aina ya muziki anaofanya kwa sasa, amesema hip hop inabadilika, na kwamba kwa sasa mwana hip hop yoyote akitaka kubamba na kuingia kwenye tuzo kama hizi anapaswa kuchanganya ladha kama alivyofanya kwenye Don Bother na Perfect Combo.
Akitoboa siri ya ngoma zake kufanya vizuri, amesema hakuna siri bali ni ubunifu, video kali na 'idea' zisizojirudia.
Kumpigia kura Joh Makini pamoja na wasanii wengine unaowakubali ingia hapa:- https://www.eatv.tv/awards