Jumatano , 9th Nov , 2016

Leo zikiwa zimebaki siku 32 kutolewa kwa Tuzo za EATV (EATV AWARDS) kampuni ya East Africa Television LTD kupitia kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio leo wametangaza wasanii wengine kumi wanaoshiriki katika vipengele viwili.

Wasanii waliotangazwa leo ni katika kipengele cha filamu bora ya mwaka na kipengele cha muigizaji bora wa kike.

Mkuu wa Matukio wa Baraza za Sanaa Tanzania (BASATA), Kurwijira Maregesi alitaja majina matano ya wasanii wanaowania kipengele cha muigizaji bora wa kike (na jina la filamu kwenye mabano) kuwa ni 

Nominee: Chuchu Hansy (Laura)

Nominee: Khadija Ally (3 Days)

Nominee: Frida Kajala Masanja (Hii ni laana)

Nominee: Rachael Bitulo njingo (Nimekosea wapi)

Baada ya kutangazwa kwa washiriki hao katika kipengele cha muigizaji bora wa kike, mwakilishi kutoka Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude ambao ni wadhamini wakuu wa tuzo za EATV AWARDS kwa kushirikiana na Coca Cola aliweza kutaja majina matano ya wasanii wengine ambao wanawania tuzo katika kipengele cha filamu bora ya mwaka kama ifuatavyo.

Filamu iliyoingia- Safari ya gwalu

Filamu iliyoingia- Hii ni laana

Filamu iliyoingia- Mfadhili wangu

Filamu iliyoingia- Nimekosea wapi

Filamu iliyoingia- Facebook profile

Tags: