Ommy ambaye ameweka rekodi ya kulitikisa jiji la London kwa onyesho kali alilolifanya siku ya wapendanao, amedokeza kuwa PKP imejipanga kwa ajili ya mambo makubwa kabisa katika siku zijazo, na hangependa kumwaga mchele wote kwa sasa kabla mipango hii haijakamilika.
Tayari Ommy amekwishatoa sehemu ya mavazi ya PKP akimaanisha Poz Kwa Poz na hivi karibunia amesema kuwa atafanya uzinduzi mkubwa kutambulisha mpango huu kwa watu.