
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba Zacharia Hans-Pope amesema, Yanga walikuwa na uwezo mkubwa wa kushindwa lakini kilichowakosesha ushindi katika mchezo huo ni uoga kwani walifanya mashambulio ya maana mara chache katika lango la wapinzani wao na mara zote walikuwa wakipiga mipira ya mbali ambayo ilikuwa haina maana.
Pope amesema, Mo Bejaia sio timu nzuri sana kwani katika kipindi cha pili Yanga walikuwa na uwezo wa kusawazisha na hata kupata bao la pili la ushindi lakini walipoteza uwezo wa kutokujiamini.
Pope amesema, kwa nafasi waliyonayo Yanga kufanya vizuri labda kwa timu ya Medeama ya nchini Ghana lakini wakiongeza juhudi pia wanaweza kufanya vizuri zaidi mbele ya TP Mazembe ambayo itakutana nayo Juni 28 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam pamoja na katika mchezo wa marudiano dhidi ya Mo Bejaia.
Yanga walikubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Mo Bejaia mchezo uliopigwa Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia nchini Algeria.