Jumatano , 13th Apr , 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehitimisha ziara yake mkoani Lindi, huku msafara wake ukizuiawa na wanakijiji cha kiwalala, waliofunga barabara ili wafikishe ujumbe wao wa kutokamilika kwa mradi wa kilimo cha Umwagiliaji.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi katika ziara yake Wilayani Ruangwa

Wakizungumza kijijini hapo wakazi hao wamesema kuwa mradi huo ambao ulianza mwaka 2010 na kutakiwa kukabidhiwa mwaka 2011 lakini hadi leo mradi huo haujakamilika hali inayowafanya kushindwa kulima kwa tija.

Kufuatia malalamiko ya wakulima hao Waziri Mkuu Majaliwa alitoa maagizo kwa mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, kuambatana na wataalamu wa kilimo ili kubaini changamoto zinazosababisha kutokamilika kwa mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amesema kuwa atalishughulikia suala hilo kama alivyoagizawa na endapo kuna mtu au watu watabainika kula hela za mradi huo basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Sauti Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akitoa maelekezo kwa Mkuu wa mkoa wa Lindi kuhusu mradi wa Kilimo cha umwagiliaji