Jumatatu , 4th Apr , 2016

Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Rukwa, imetoa maelekezo kwa matawi yote ya kata na vijiji wilayani humo kuwa na mpango endelevu wa kuwa na ratiba ya kutekeleza shughuli mbalimbali za Maendeleo.

Katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa rukwa Clemence Bakuli akiongea na viongozi wa jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Rukwa.

Akizungumza na wanajumuiya hao Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilayani,Sumbawanga, Evance Nachimbinyia, amesema kwa kuadhimisha siku hiyo katika shughuli za maendeleo itatatu kwa sehemu kubwa matatizo yanayowakabali wananchi wa sehemu husika.

Nachimbinyia, amesema kuwa wataanza kusaidia kwa vikundi kwa kuleta maenendeleo katika kata, vijiji, hadi wilaya na baadae wataanza kusaidi mmoja mmoja kuhakikisha kila mwanajumuiya aweze kumiliki nyumba.

Nao baadhi ya wanajumuiya waliojitokeza katika kufanya shughuli hizo za maendeleo wamesema kuwa kwa kutekeleza kauli mbiu ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, “HAPA KAZI TU”wameona hakuna haja ya kufanya mikutano mingi isiyokuwa na tija na badala yake ni bora wajikite katika shughuli za maendeleo.

Jumuiya hiyo imewataka viongozi wote kuwa wazalendo kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake za kuleta maendeleo ya kweli na ya haraka katika jamii.