Jumanne , 29th Mar , 2016

Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu nchini Tanzania-Sumatra, imeanza kuendesha zoezi la ukaguzi na ukamataji wa daladala zinazokiuka leseni ya usafirishaji ambapo kwa kipindi cha siku tatu zilizopita jumla ya daladala 105 zimekamat

Msemaji wa Sumatra Bw. David Mziray

Msemaji wa Sumatra Bw. David Mziray amesema daladala hizo zimekamatwa kwa makosa mbali mbali mojawapo ikiwa ni kukatiza ruti, kuongeza nauli kiholela pamoja na lugha chafu na kwamba zoezi hilo la ukaguzi limekuwa likifanywa kwa kushirikiana na jeshi la polisi ambapo wahusika wake wamewekwa nguvuni.

Mziray amefafanua kuwa kati ya daladala hizo, 36 tayari wahusika wake wameshafikishwa mahakamani katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni na kwamba hatua ya kuwafikisha huko inatokana na kusitisha kwa muda utaratibu wa faini baada ya wamiliki wa vyombo vya usafiri kufungua kesi kupinga utaratibu wa faini.

Ameongeza kuwa wao kama wasimamizi wa sekta ya usafirishaji nchini wamelazimika kufikia hatua hiyo baada ya huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam kuonekana kama haina usimamizi kutokana na walipewa dhamana ya kuviendesha vyombo hivyo kujifanyia mambo kiholela hasa nyakati za jioni ambapo mahitaji ya usafiri yamekuwa makubwa.