Jumatatu , 2nd Jun , 2025

Mshindi mara mbili wa tuzo ya MVP A'ja Wilson mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na kiwango bora msimu huu na kuisaidia timu yake kuzidi kufanya vizuri kwenye ligi ya mpira wa kikapu upande wa wanawake nchini Marekani WNBA

A'ja Wilson

Nyota huyo wa Las Vegas Aces msimu Jana alifanikiwa kupata tuzo ya mchezaji bora wa mashindano na  kutengeneza rekodi mchezaji wa kwanza kufunga alama 1000 kwa msimu mmoja

A'ja Wilson amefunga alama 19 na kupora mipira mitatu kwenye mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia Leo timu yake iliposhinda vikapu 75-70 dhidi ya Settle Storm ukanda wa Magharibi WNBA