Alhamisi , 29th Mei , 2025

Kocha mkuu wa timu ya Okhlahoma City Thunder inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu nchini Marekani ukanda wa magharibi  Mark Daigneaut amefanikiwa kuipeleka Thunder kwenye  fainal ya NBA  baada ya miaka kumi na tatu kupita 

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 amekua na mafanikio toka alipokua kocha mkuu wa timu hiyo mwaka 2020 Mark Daigneaut msimu jana alishinda tunzo ya kocha bora wa mwaka msimu huu ameingoza vyema Oklahoma City Thunder kushinda michezo 64 nakupoteza 14 

Thunder  wamefanikiwa kwenda fainal ya NBA mara baada ya kupata ushindi wao wanne kati ya michezo mitano waliocheza  dhidi ya Minnesota Timberwolves  ukanda wa magharibi ivyo wanasubiri mshindi kutoka uķanda wa mashariki ambapo mpaka sasa Indiana Pacers anaongoza kwa ushindi  wa michezo mitatu mbele ya New York Knicks alieshinda mchezo mmoja tu