Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema, katika kambi hiyo wataendelea kumkosa Mshambuliaji Donald Dombo Ngoma ambaye yupo kwako nchini Zimbabwe katika msiba wa mdogo wake lakini mshambuliaji Amis Tambwe ambaye aliumia katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Cercle de Joachim ataungana na kikosi kwa ajili ya kambi ya visiwani Pemba.
Mwambusi amesema, wameamua kurudi tena visiwani Pemba kuweka kambi kutokana na hali ya utulivu iliyopo ndani ya visiwa hivyo ambayo iliwapa matokeo mazuri.
Mwambusi amesema, wanachokiona mbele yao wana mechi ngumu mfululizo zipo karibu sana lakini wanachokihitaji ni kupambana na Azam FC ili kuweza kutetea nafasi yao ya Ubingwa wa ligi kuu ambao wanaushikilia ili kuweza kuurejesha tena.