Wakitoa maoni yao katika ukurasa wa Facebook wa East Africa Television wananchi hao wamesema kauli hiyo ya Rais Magufuli haikuwa sahihi, na wengine kumtaka atengue kauli yake kwani walimchagua kama Magufuli na sio chama.
"Hahahaaa ni kweli katumwa na CCM na ndo wamempa mbinu zote za maigizo na scripts zote... sijapendezwa sana Rais wangu kwa kauli hiyo.... Atengue kauli please!! Wengine tulichagua yeye kama Magufuli ila sio yeye kama mgombea wa ccm... I hate CCM and all members wa hicho chama... Kama na yeye yuko kichama zaidi, hatutavutiwa naye pia”, alisema Revocatus Obote.
Mdau mwengine aliendelea na maoni haya...
“Ameshabadlisha kauli yake tayari, ni kazi ambayo ametumwa na CCM sio wananchi tena, sasa kama ni kweli anataka kufanya kazi aliyotumwa na ccm inamaanisha kuja kumalizia pale alipoacha huyo wa Chalinze, kuja kuimalizia nchi yenyewe sasa”, alisema Kannole Kaisy.
Mdau mwengine alisema kutokana na kauli imeonyesha ni tatizo la kuchagua viongozi ambao sio vijana, na kushauri kuwapa nafasi vijana ili kupata fursa ya kuliongoza Taifa, ikiwemo na kubadili katiba ya nchi.
“Aseee yani hii nchi inaendeshwa kichama sio, kwahiyo CCM ndo anaiongoza na sio wananchi wa Tanzania, hili ndo tatizo la kuchagua wasio vijana siku hizi, kuna low expentance sasa hii katiba inabidi ibadilishwe ili vijana wapate fursa za kugombea urais, unajua sisi atuendelei kutokana kila secta unakuta mzee ndo anaongoza, tuwaige wenzetu basi yani Tanzania kila kitu bàdo tuko nyuma, dah yani bora kuzamia ulaya tu kwa mambo kama haya, we bado ufikilie jinsi ya upatikanaji wa ajira kwa vijana na mambo mengine ya nchi unaongoza chama sasa we unadhani na mtafaruku unao endelea nchini we unadhani vijana hawatojiunga kwenye makundi ya ajabu”, alisema mdau aliyejulikana kwa jina la Cannibal Man.
Jana kwenye sherehe za kutimiza miaka 39 chama cha mapinduzi (CCM), Rais Magufuli alisema ataendelea kufanya kazi aliyoagizwa na CCM, kauli ambayo imeleta minong'ono mingi miongoni mwa Watanzania.