
Michuano ya vijana ya tennis iliyoandaliwa na chama cha tennis Tanzania TTA imehitimishwa hii leo katika viwanja vya klabu ya Gymkhana jijini Dar es salaam kwa michezo mbalimbali ya fainali kupigwa ikihusisha vijana wa chini ya miaka 12 na 10.
Mratibu wa michuano hiyo Fouard Somi ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TTA amesema kuwa kwa kiasi kikubwa lengo la chama kutafuta vipaji vipya na kupata wachezaji wenye ubora katika michuano hiyo limefanikiwa na wanatoa pongezi kwa wazazi kwa kuwaleta watoto wao kushiriki michuano hiyo iliyofanyika kwa siku mbili ikianza hapo jana ikishirikisha pia wachezaji kutoka mikoa mingine ya Tanzania.