Mkuu wa Wilaya ya Longido Ernest Kahindi.
Wakiongea kabla ya kuanza kwa baraza la madiwan wa halmashauri hiyo baadhi ya wananchi akiwemo bi Sinyati Eliasi ,amesema kwa kipindi kirefu licha ya ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na vongozi mbalimbali wameendele kutaabika matatizo yao, lakini wanaamini kwa kasi iliyopo kupitia madiwani wao watapatiwa suluhisho la kudumu.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido Sabone Kenedy pamoja na Makamu wake Esupat Kiloriti wamesema kuwa kwa sasa wanakazi moja ya kuwatumikia wananchi badala yakuendekeza itikadi za vyama vyao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Longido Ernest Kahindi amewatak amadiwani kuwatumikia wananchi na kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na wananchi wengi badala ya kufanya malumbano yasiyo na tija.
Wilaya ya Longido ni moja kati ya wilaya zinazokabiliwa na ukame licha ya kuwa na idadi kubwa ya mifugo , hivyo juhudi zinahitajika kulinda mazingira pamoja na kukuza shughuli mbadala hasa katika kipindi cha ukame .