
Kabla ya kuhamishiwa Babati, Natty alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,ambapo Sagini alitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam na kuagiza mkurugenzi huyo kurejea Dar es Salaam.
“Pamoja na kusimamishwa kazi, Natty anapaswa kurudi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kusubiri uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili", alisema Jumanne Sagini
Tuhuma zinazomkabili Natty ni pamoja na usimamizi mbaya uliosababisha barabara za Manispaa ya Kinondoni kujengwa chini ya kiwango, na kutochukua hatua kwa watendaji wa manispaa waliokuwa chini yake.
Sagini alisema tuhuma nyingine zinazomkabili Mussa Natty ni ukosefu wa uadilifu katika ubinafsishaji wa eneo la ufukwe wa bahari eneo la Coco Beach, na malalamiko ya wananchi juu ya viwanja katika eneo la Kinondoni, ulioambatana na usimamizi duni wa watumishi hasa sekta ya mipango miji na ardhi.