Jumatano , 12th Nov , 2025

Makamu mwenyekiti wa cha Chama cha demokrasia na Maendeleo, John Heche, ameiomba mahakama kuharakisha mchakato wa kusikilizwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu.

Makamu mwenyekiti wa cha Chama cha demokrasia na Maendeleo, John Heche, ameiomba mahakama kuharakisha mchakato wa kusikilizwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu mara baada ya kuahirishwa leo Novemba 12 hadi pale msajili wa Mahakama atakapopanga tarehe ya kusikilizwa tena.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari, Heche amezungumzia pia watu waliokamatwa na kusema kuwa wamewaandalia wanasheria wa kuwasimamia katika maeneo yote nchini. Ameongeza kuwa ni lazima uchunguzi huru na wa haki ufanyike kuduatia matukio ya Oktoba 29,2025.

Kesi hiyo imeahirishwa baada ya Mshitakiwa Tundu Lissu kuweka pingamizi dhidi ya upande wa Jamhuri kwa shahidi wa nne wa siri (Witness chamber) atokee kizimbani kwani Shahidi huyo kutoa ushahidi wa siri si salama kwake kama mshitakiwa.

Katika pingamizi hilo,Lissu alichukua muda wa masaa mawili kutoa kanuni sita zinazokataza shahidi wa siri ikiwemo kanuni za ulinzi wa mashahidi za mwaka 2025, ambapo amesema kiboski ambacho shahidi yupo ni kizimba maalum cha ushahidi ambacho hata majaji hawatamuona katika kutoa ushahidi au kumuona isipokuwa mawakili pekee wa Serikali.

Baada ya pingamizi hilo upande wa Jamhuri kupitia kwa Nassoro Katuga ulisema hoja za mshitakiwa zilikuwa nyingi na kuomba majaji na Mshitakiwa wawape muda wa kupitia kanuni hizo,ombi ambalo lilikubaliwa na Mshitakiwa Tundu Lissu na majaji.

Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Dkt. Rugemeleza Nshala amefafanua pingamizi la mshtakiwa Tundu Lissu kwa kusema kuwa shahidi ambaye anatakiwa kufichwa ni lazima aonekane mbele ya jaji akiwa kizimbani.

Dkt. Shala ametoa kaulio hiyo mbele ya waandishi wa Habari waliohudhuria katika kesi hiyo leo Novemba 12,2025, na kufafanua kuwa kanuni zinamtaka shahidi aonekane mbele ya jaji ili kuepusha kutolewa kwa Ushahidi wa kubambikiza.