Jumatano , 12th Nov , 2025

Bunge la 13 limeanza jana Jumanne, tarehe 11 Novemba 2025, likianza na uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha kiapo cha uaminifu na ahadi ya uzalendo kwa wabunge wateule, zoezi ambalo limehitimishwa siku ya leo. 

Kikao cha Tatu cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 kitakachofanyika kesho Alhamis Novemba 13, 2025 kimepangwa kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sambamba na uchaguzi na uapisho wa Naibu Spika wa Bunge.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ametangaza hatua hiyo leo, tarehe 12 Novemba 2025, wakati akiahirisha kikao cha pili cha Bunge, Jijini Dodoma na kuwataka wabunge wote kuhudhuria kikao hicho bila kukosa, kutokana na uzito wa ajenda zilizopangwa kujadiliwa.