Waziri wa Kilimo,Uvuvi na Mifugo nchini Tanzania Mwigulu Nchemba atoa masaa 48 kuanzia leo kwa Kampuni ya Sparkway LTD kulipa shilingi Bilion 3.4 kwa wakulima wa Korosho wa mkoa wa Pwani na baada ya malipo hayo kufanyika wakulima wataanza kulipwa pesa zao siku ya jumatatu ijayo kwa utaratibu maalumu uliowekwa na wakulima hao pamoja na serikali.
Waziri Nchemba ameyasema hayo leo mkoani Pwani kwenye kikao cha dharura alichokifanya kwa kuwakutanisha watumishi mbalimbali wa serikali,wauzaji na wanunuzi wa korosho nchini baada yakupokea malalamikom mengi yakudhulumiwa fedha zao na wanunuzi wakubwa ambao wanapeleka Korosho nchi za nje.
Waziri amewaonya wafanyabiashara wakubwa kuacha tabia yakucheza na fedha za wafanyabiashara wadogo hasa wakulima kwani wanatumia gharama kubwa kuzalisha chakula lakini fedha wanazolipwa ni ndogo na kuacha mazoea ya ufaanyaji biashara usiofwata sheria maalum za ununuzi.