Jumatano , 26th Mar , 2014

Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Kenya, Amani amekataa kuweka wazi mipango ya muziki wake pamoja na usimamizi wake.

Amani

Hii ni baada ya lebo ya Ogopa ambayo amefanya nayo kazi kutoka mwaka 1999 alipoanza biashara ya muziki, kusitisha mikataba na wasanii wake wote mwanzoni mwa mwaka.

Amani amesema kuwa, hawezi kujadiliana kuhusiana na suala hili katika wakati huu bila kuweka
wazi sababu ya kufanya hivyo, ingawa imefahamika kuwa kwa sasa yupo katika mpango wa kurejea kwa mara nyingine katika muziki kwa kishindo.

Amani wiki kadhaa zilizopita, pia alinukuliwa akisema kuwa, ni kitu kizuri kukaa nje ya muziki
kwa muda ili kuweza kuweka mpango mzuri wa kurudi vizuri.

Tags: