Moalin alijiunga na KMC FC kutokea Azam FC alikofukuzwa kazi Augosti 29 2022.Raia huyo wa Marekani alitoa sababu tano zilizomfanya kuondoka KMC FC ikiwa bado mapema mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara kutokana na kushindwa kuvumilia mazingira ya kazi kwenye kikosi hiko.
Malacia amekaa nje ya uwanja tangu aitumikie timu ya taifa ya Uholanzi dhidi ya Crotia mchezo wa mashindano ya ligi ya mataifa ya bara la Ulaya uliofanyika mwaka 2023.Baada ya hapo Mchezaji huyo amekuwa muhanga wa matatizo ya goti yanayomsumbua mara kwa mara kurejea kwake uwanjani mwezi Februari kuliahirishwa kutokana na kuhofia kumuharakisha kurudi uwanjani na kutonesha jeraha lake.
Mchezaji huyo kaitumikia timu yake michezo 16 mchezo wake wa mwisho ukiwa Oktoba 6 siku moja kabla ya kupata ajali ya gari akiwa na Rafiki zake.Kaitumikia michezo 3 timu yake ya taifa mchezo wake wa kwanza ukiwa ule wa Novemba 22 dhidi ya Iraq ambao ulitamatika kwa suluhu ya kutokufungana.
Huu ni mwanzo bora wa ligi ya kikapu Marekani NBA tangu msimu wa 2015-16 klabu ya Golden State Warriors iliyocheza michezo 24 mfululizo kwenye msimu huo.Donovan Mitchell amekuwa kwenye kiwango bora sana msimu kwa Cavaliers kamaliza mchezo wa jana akiwa amefunga alama 36 na Wachezaji wengine watano wamefikisha alama zaidi ya kumi mchezo wa jana huku ikitoka nyuma kwa alama 9 robo ya tatu na kushinda mchezo huo.
Sababu mbalimbali zimetajwa juu ya uamuzi uliochukuliwa na Uongozi wa timu hiyo kuhamia uwanja wa KMC Complex ikiwemo picha za vidio ambazo hazina uthibitisho kama kweli zinaihusu klabu hiyo zikionyesha mabomba ya sindano uwanjani Azam Complex ikisemekana Wachezaji wake wanaongeza nguvu kwa kuchoma sindano.
Msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A baada ya michezo 12 kuchezwa.
Ushindi wa goli nne kwa sifuri dhidi Osasuna mchezo uliopigwa uwanja wa Santiago Bernabéu Stadium siku ya Jumamosi ya Novemba 9 mchezo huo ulitamatika huku kukiwa na majeruhi wapya kwa kikosi cha mabingwa watetezi wa La liga, Eder Militao atakaa nje ya uwanja miezi 9 baada ya kuumia goti, Rodrygo Goes na Lucas Vazquez wote walipata majeraha kwenye mchezo huo.
Kikosi cha Liverpool msimu 2024-25 kinapewa nafasi ya kuwa mabingwa wa Ligi kuu Uingereza EPL msimu huu.
Yanga itashuka tena dimbani baada ya lenda ya FIFA kukabiliana na Al Hilal katika mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika mchezo utakaochezwa Novemba 26 2024.Baada ya kupokea kipigo dhidi ya Tabora United kuna taarifa nyingi zilienea kwenye vijiwe vya mpira na mitando ya kijamii kuhusiana na Kocha wa timu hiyo kuwekwa kitimoto na Uongozi wa kikosi cha Wananchi.
Kipigo cha jana kwa Wajangwani kimekuwa cha pili mfululizo baada ya kuruhusu kufungwa goli 1-0 dhidi ya Azam wiki iliyopita. Hii inakuwa mara ya kwanza Yanga SC kupoteza michezo miwili mfululizo tangu mwaka 2020.
Tchakei alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo kwa mwezi Oktoba akiwashinda Lusajo Mwaikenda wa Azam FC na Pacome Zouzoua wa Yanga, alioingia nao fainali katika mchakato wa tuzo za mwezi uliofanywa na Kamati ya tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa mwaka wa 2027 yanatarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ushirikiano nchi tatu Tanzania, Kenya na Uganda ambazo ndizo zitakuwa nchi wenyejiwa mashindano hayo.
Nyota huyo wa zamani wa K.R.C. Genk ya Ubelgiji, TP Mazembe ya Congo DR na Aston Villa ya England kumbukumbu nzuri ya maisha yake ni kufunga goli dhidi ya Manchester City mahasimu wa United kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Carabao mwaka 2020.
Takwimu za mechi mbili walizokutana zinaonyesha timu ya Wananchi imeshinda michezo yote miwili dhidi ya Wapinzani wao siku ya leo (3-0, 1-0) Tabora United kutokea Tabora ambayo inashika nafasi ya 10 ikiwa imevuna alama 14 msimu huu.
